KIDATO CHA NNE 2022
102/3- KISWAHILI – Karatasi ya Tatu
FASIHI- 2022- Muda: – Saa 2
1.SEHEMU YA ‘A’: USHAIRI (LAZIMA)
Eti
Mimi niondoke hapa
Niondoke hapa kwangu
Nimesaki, licha ya risasi
Vitisho na mauaji, siondoki
Mimi
Siondoki
Siondoki siondoki
Niondoke hapa kwangu!
Kwa mateke hata na mikuki
Marungu na bunduki, siondoki
Hapa
Siondoki
Mimi ni Pahame!
Niondoke hapa kwangu!
Fujo na ghasia zikizuka
Na kani ya waporaji, siondoki
Haki
Siondoki
Kwangu siondoki
Niondoke hapa kwangu!
Nawaje; waje wanaokuja
Mabepari wadhalimu, siondoki
Kamwe
Siondoki
Ng’oo hapa kwangu!
Katizame chini mti ule!
Walizikwa babu zangu, siondoki
Sendi
Nende wapi?
Si hapa kitovu changu
Niondoke hapa kwangu
Wangawa na vijikaratasi
Si kwamba hapa si kwangu, siondoki
Katu
Siondoki
Sihitaji karatasi
Niondoke hapa kwangu
Yangu mimi ni ardhi hii
Wala si makaratasi, siondoki
Maswali
a) Shairi hili ni la aina gani? Kwa nini? (alama 2)
b) Taja masaibu anayopitia mzungumzaji. (alama 4)
c) Eleza toni ya shairi hili. (alama 2)
d) Eleza muundo wa shairi hili. (alama 3)
e) Tambua matumizi ya mbinu ya usambamba. (alama 2)
f) Andika ubeti wa tano kwa lugha nathari . (alama 4)
g) Tambua idhini moja ya mtunzi. (alama 1)
h) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi. (alama 3)
(i) karatasi
(ii) nimesaki
(iii) kitovu
SEHEMU YA B:TAMTHILIA: Kigogo, P. Kea
2. “Na hiyo sauti ya Jabali imekuwa adha. Inanikama roho….”
- Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
- Tambua mbinu mbili za lugha zilizotumika dondooni. (alama 2)
- Kwa hoja kumi na nne fafanua matendo yanayomkaba roho msemaji. (alama 14)
3. Eleza athari kumi za tamaa na ubinafsi kwakurejelea tamthilia ya Kigogo. (alama20)
SEHEMU YA C:RIWAYA: Chozi la Heri, A. Matei
4. “Sisi tunataka kiongozi yeyote, awe mwanamke au mwanamume, atakayewezakulielekeza jahazi hili letu kwenye visiwa vyahazina.”
a) Eleza muktadha wadondoo hili. (alama 4)
b) Bainisha mbinu nne za lugha zinazojitokeza katikadondoo hili. (alama 4)
c) Huku ukirejelea riwaya Chozi la Heri, jadili mchango wa warejelewa katikakuboresha maisha ya Wahafidhina kwa hoja kuminambili. (alama 12)
5. a) “Na kuwe huko kumtoa mekoni lakini hili la kumpa jukumu la kuliongoza jamii nzima! Itakuwa kukivika kichwa cha kukukilemba.”
(i) Bainisha toni inayojitokeza katikadondoohili. (alama 2)
(ii) Linganisha na ulinganue msemaji na msemewa katikadondoohili. (alama 9)
b)Changanuamtindo katika dondoo hili. (alama 9)
“Kumbe wewe ni sawa na yule Mwangeka wa kihistoria ambaye kivuli chake kikitembea siku zote mbele yake, ambaye mwili wake ulikuwa kaka tu,roho yenyewe iliishinje ya kaka hili kwa kutotaka kuthibitiwa? Umewezaje kunusurika? Kumbe huo wadhifa waliokupa wa kwenda kudumisha amani Mashariki ya Kati umetokea kuwa wongofu wako? Maskini Lily mkaza mwanangu! Umekuwa kama jani linalopukutika msimu wa machipuko! Umetoweka katika ulimwengu huu ukiwa teketeke, hata ubwabwa wa shingo haujakutoka!”
SEHEMU YA D: Hadithi Fupi
A. Chokocho na D. Kayanda(Wahariri), Tumbona Hadithi na NyingineLisiloshiba
Jibu swali la 6 au 7
6.Ukirejelea hadithi zifuatazo, eleza jinsi maudhui ya mapenzi na asasi ya ndoa yanavyojitokeza. (alama20)
a)Mapenzi ya Kifaurongo
b)Masharti ya Kisasa
c)Ndoto ya Mashaka
d)Mtihani wa Maisha
7. Salma Omar Hamad,Shibe Inatumaliza
a) “Wanafanya kazi ya ukwe tu. Hawana wasichofanya lakini hawanawafanyacho.
i) Bainisha tamathali tatu za usemi zinazojitokeza katikadondoohili. (alama 3)
ii) Kwa hoja zozote nane, thibitisha ukweli wa kauli iliyokolezwa huku ukirejeleahadithi Shibe Inatumaliza.(alama8)
Alifa Chokocho,Tulipokutana tena
b)‘Pale nilipokwenda kulelewa palikuwa jahanamukwangu.”
Tathmini ukweli wa maneno haya ukirejelea hadithi ‘Tulipokutana Tena’. (alama 9)
SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI
- a) Eleza maana ya vipera vifuatavyo vya fasihi simulizi. (alama 8)
(i)misimu
(ii)ngomezi
(iii)miviga
(iv)maapizo
b) (i) Fafanua dhima sita za miviga katika jamii yako. (alama 6) (ii) Tambulisha sifa zozote sita za misimu. (alama 6)
Huu ndio ukurasa wa mwisho uliopigwa chapa maswali.
………………………………………………………………………………………………………