Swali la Kwanza
Tahariri kuhusu kutelekezwa kwa wakongwe na suluhu yake
Sura
i) Iwe na sura ya jina la gazeti, siku na tarehe.
ii) Iwe na mada yake.
iii) Mwili/maelezo yahusu jinsi wakongwe wanavyotelekezwa na mapendekezo ya suluhu.
iv) Iwe na hitimisho kama vile kauli ya heshima, sahihi na jina la mwandishi.
Maudhui
a) Utelekezaji wa wakongwe unadhihirika kwa namna mbalimbali kama:
i) kutothaminiwa na jamaa zao
ii) kukosa kutibiwa wanapougua
iii) kushukiwa kuwa ni wachawi
iv) kuchukuliwa kuwa mzigo
v) kuachwa kuishi katika makao duni
vi) kuachwa katika umasikini
vii) kukosa kupewa chakula (bora)
vii) kunyimwa mavazi/malazi bora
viii) kutengwa vijijini/ kuishi maisha ya upweke
Suluhu
i) Wakongwe wapewe msaada.
ii) Makazi ya wakongwe yajengwe kupitia serikali na mashirika ya kijamii na kidini.
iii) Serikali iimarishe mpango wa kutoa hela kwa wakongwe kila mwisho wa mwezi.
iv) Wanajamii wahamasishwe kuwajali wakongwe wao katika kiwango cha familia.
v) Wanajamii wapewe mafunzo kuhusu namna ya kupanga maisha yao ya uzeeni.
vi) Hazina ya bima ya afya iimarishwe ili kuwajumuisha wakongwe wote.
vii) Wanajamii wapewe hamasisho kuhusu jinsi ya kuwatunza wakongwe.
viii) Imani hasi za kishirikina kuhusu wakongwe zipigwe vita na wanajamii na walinda sheria.
Swali la Pili
Jinsi ya kudumisha umoja wa kitaifa
i) kupiga vita ukabila na vitendo vinavyotukuza kabila/ubaguzi
ii) Kuwe na elimu kuhusu utaifa.
iii) Wananchi wawe na uhuru wa kuishi mahali popote nchini Kenya.
iv) Wananchi waruhusiwe kufanya kazi popote nchini.
v) Maendeleo yasambazwe kote nchini kwa usawa.
vi) Viongozi wahubiri umoja/mshikamano wa kitaifa.
vii) Serikali ibuni sera za jinsi ya kudumisha umoja wa kitaifa.
viii) Kiswahili kiimarishwe kwa sababu ni lugha ya kitaifa.
ix) Vyombo vya habari vihamasishe umoja wa kitaifa.
x) Jamii ihimizwe kupendelea ndoa za mesto.
xi) Wachochezi wa uhasama baina ya jamii mbalimbali waadhibiwe.
xii) Ubaguzi katika ajira uepukwe.
xiii) Asasi za kijamii zipige vita ufisadi.
Swali la Tatu: Methali: Ukupigao ndio ukufuanzao.
Maana:
Unajifunza jambo baada ya kupata kichapo fulani. Mtu hupata funzo baada ya kupitia katika changamoto fulani maishani.
Mtahiniwa atunge kisa kuonyesha ukweli wa methali hii. Kisa kionyeshe pande zote mbili za methali yaani ‘kupigwa’ na ‘kufunzwa.’
Mifano ya baadhi ya visa vinavyoweza kutungwa:
i) mwanafunzi aliyefanya kosa fulani kisha baada ya kuadhiniwa anapata funzo na kubadilika,
ii) msichana aliyeambulia ujauzito akiwa bado mwanafunzi na baadaye akawa na tahadhari asiambulie ujauzito
iii) tukio la jamii kuathiriwa na ugonjwa fulani kisha wenyeji wake wakapata funzo na kuepukana na vitendo vilivyosababisha ugonjwa huo kama njia ya kujizuia kuathiriwa tena,
iv) mfanyakazi mzembe kazini anapigwa kalamu halafu anajifunza na kuepukana na ugoigoi wake
Swali la Nne: Mdokezo tamati
… sitawahi kumwamini mtu nisiyemjua vyema.’
Mtahiniwa atunge kisa ambacho mwishoni mwake mna maneno haya.
Kisa kionyeshe sababu za msemaji kutoa kauli hii. Mtahiniwa ajihusishe katika kisa hiki. Msemaji awe alipatwa na athari hasi kutokana na tukio fulani kama vile kusalitiwa na mtu fulani asiyemwelewa vyema. Aidha, kisa kionyeshe athari za kumwamini mtu asiyemfahamu vyema.
Baadhi ya visa vinavyoweza kurejelewa ni:
i) kuibiwa
ii) kunajisiwa
iii) kulaghaiwa/kutapeliwa
iv) kupotoshwa njia kwa kisingizio cha kuelekezwa mahali pageni
v) kuolewa/kuoa kisha kuachwa ghafla
Tanbihi
i) Asiyemaliza kwa mdokezo huu achuliwa kuwa ana udhaifu wa kimtindo wala sio kupotoka.
ii) Anayeanzia mdokezo lakini kisa kilenge maudhui atakuwa amelenga/amejibu swali.
iii) Anayekosa kutumia maneno ya mdokezo lakini kisa kimelenga, amejibu swali vilevile.