KISWAHILI LUGHA
KIDATO CHA NNE 2022
AGOSTI 2022
MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA
(SIRI)
(Mwongozo huu una kurasa 9 zilizochapishwa)
Hakimiliki: Mwongozo huu ni kazi asilia ya mtayarishi. Hivyo basi sio tendo la kiungwana kuzalisha Mwongozo huu kwa njia yoyote bila kuomba na kupewa idhini ya mtunzi.
1. SWALI LA KWANZA: UFAHAMU (ALAMA 15)
a) Athari za mikakati ya kukukamilisha mitaala kwa wanafunzi
(i) Vipindi vya masomo vilianza mapema sana (alfajiri).
(ii) Vipindi vya masomo viliendelea na kupita saa kumi jioni.
(iii) Wanafunzi walikosa muda wa kushiriki michezo ya baada ya madarasa.
(hoja 3 x 1 = alama 3)
b) Changamoto za katika kutekeleza shughuli zao
(i) Hali ya barabara ni mbovu. Haijabandikwa lami.
(ii) hali ngumu ya hewa. – Kuna manyunyu ya mvua na baridi.
(iv) kulazimika kukanyaga ardhi mbichi (matope) kwa miguu kavu – Mutia amevua viatu ili
aweze kupita matopeni.
(v) Vyombo vya usafiri viko katika hali duni. Pikipiki ya Mwalimu Bidii ina magurudumu
yaliyoisha kwani hayana meno.
(vi) mwendo mrefu kufika mahali pa kufanyia kazi – Kilomita kumi ni mwendo mrefu.
c) Ithibati kwamba uamuzi una athari zake kwa kuwazingatia wananchi
(i) Walihongwa ili kuwachagua viongozi.
(ii) Waliwachagua viongozi kwa kuzingatia uhusiano; watu wao.
(iii) Hawakushiriki katika kupiga kura kuwachagua viongozi wao.
(hoja 3 x 1 = alama 3)
d) Kisawe cha bughudha kutoka kifunguni
usumbufu (msitari wa mwisho katika aya ya kwanza)
(1 x 1 = alama 1)
e) Visawe vya nahau
(i) aliyejitolea mhanga
(ii) kisiende upogo/mrama/fyongo
(2 x 1 = alama 2)
f) Maana ya ‘Hakuwa na kaba ya ulimi’ pasipo kukanusha
Angesema lolote.
(1 x 1 = alama 1)
g) Methali inayoasa kuhusu ulimi
Ulimi hauna mfupa.
(1 x 1 = alama 1)
2. SWALI LA PILI: UFUPISHO (ALAMA 15)
a) Hoja katika aya mbili za kwanza
(i) Katika karne ya kumi na tisa Afrika ilivamiwa na Ulaya na kutwaliwa.
(ii) Mataifa mengine yaliyodhaniwa kwa hayajastarabika yaliingiliwa.
(iii) Uingereza ilijitwalia nchi nyingi kwa sababu ilistawi zaidi ya mataifa mengine ulimwenguni.
(iv) Waigereza ndio walitakadamu vyombo vya usafiri wa majini.
(v) Mataifa mengine ya Ulaya pia yaling’ang’ana kumega (kupata) koloni ulimwenguni.
(vi) Uvamizi ulidhihirika kupitia utwaliwaji wa mamlaka katika mataifa yaliyoathiriwa.
(vii) Mtindo huu ulikinzana na tawala asilia za Kiafrika.
(viii) Falme zilisambaratishwa.
(ix) Hawakutathmini jinsi kila jamii iliendesha serikali yake chini ya viongozi wake/ Walipuuza mifumo ya kiutawala ya wenyeji/ Walidai kuwa wenyeji hawakuwa na mfumo wa utawala.
(x) Uhasama baina ya jamii na upekee wa mil ani mambo yaliyoangaziwa kuliko mifumo mbalimbali ya kujiongoza ya Waafrika.
(hoja 8 x 1 = alama 8)
b) Ufupisho wa aya ya tatu, nne na tano
Aya ya 3 – Athari hasi
(i) Walibuni mipaka kiholela na kutenganisha jamii moja.
(ii) Watu wa familia moja walijipata katika nchi tofauti.
(iii) Watu wa ukoo mmoja walitawanywa na kupelekwa katika nchi tofauti.
(vi) Kuna maboma yaliyopigwa mpaka katikati.
(hoja 3 x 1 = alama 3)
Aya ya 4 – Kichocheo
Uvamizi uliletwa na kutaka kunyakua maliasili iliyojaa barani Afrika.
(hoja 1 x 1 = alama 1)
Aya ya 5 – Manufaa
(i) Miundomsingi ilistawishwa.
(ii) Maeneo ya ndani ya bara la Afrika yaliweza kufikika.
(iii) Taasisi mbalimbali zilijengwa na wakoloni.
(hoja 2 x 1 = alama 2)
a — 8
b — 6
ut — 1
jumla – 15
3. SWALI LA TATU: MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
a) (i) shughuli (ii) meno
(2 x 1 = alama 2)
b) (i) /m/ na /w/ – midomoni/ mahali pa (ala za) kutamkia
(ii) /t/ na /sh/ – sighuna/hafifu/ hali ya nyuzisauti (glota) (2 x ½ = alama 1)
c) Maana za sentensi tata
(i) Mtihani ndio unaendelea wakati huu.
(ii) Mjadala kuhusu mtihani usiendelee wakati huu.
Tanbihi: Utata unatokana na kielezi ‘wakati huu’ ambapo kinaweza kurejelea chochote kati ya vitenzi viwili kwenye sentensi hiyo katika nyakati tofauti.
(2 x 1 = alama 2)
d) Kubadili tungo katika wingi
(i) Wakulima walilima cheu ili kujiandaa kwa misimu ya upanzi wa nafaka.
(ii) Mashauri yao yalituepusha na majanga ya ndwele hatari zilizosambaa haraka.
(2 x 2 = alama 4)
(Akikosea popote katika kila sentensi apewe alama 1)
e) Matumizi mawili ya ritifaa katika lugha kwa sentensi moja
(i) maneno yenye king’ong’o cha kaakaa laini
(ii) herufi/sauti zilizodondoshwa/zilizobanwa katika matamshi ya neno/ufupishaji
Mfano: Wao ‘takuwa waking’ang’ania mpira.
(2 x 1= alama 2)
Tanbihi: Lazima sentensi itumiwe katika jibu.
f) Kuandika sentensi upya kwa mujibu wa maagizo
(i)Mafunzo murua aliyopata chuoni yamemfanya Wangia kuwa (awe) stadi wa (katika) Kifaransa.
(ii) Kusherehekea kwingi kulikofanywa kulikuwa kunaadhimisha kushinda kwa Pute.
(1 x 2 = alama 2)
(iii) Shilingi elfu kumi zilitumiwa na Mari kununua simutamba mpya na kumtuza mwanafunzi bora.
(1 x 2 = alama 2)
g) Mofimu katika maneno
(i) katika – kat- mzizi, -ik- kauli na -a – kiishio
(3 alama 1, akikosea popote apewe ½)
(ii) achaguliwaye – a- shamirisho, -chagu- mzizi, -liw- kauli, -a- mzizi na -ye kirejeshi
(5 alama 2, akipata 1-2, alama ½, 3 – 4 alama 1)
h) Sentensi zenye miundo iliyopo
(i) Haendi kuungana na wanasiasa.
Ts T H N
(Sentensi sahihi 1/0)
(ii) Hilo lako lina magurudumu mapya.
W V t N V
(Sentensi sahihi yenye viungo vyote 2/0)
i) Kubainisha viungo katika sentensi
Mhandisi shupavu atakagua ujenzi wa ghorofa hatua kwa hatua.
kiima kiarifu chagizo
(j) Kueleza matumizi ya kiambishi -o katika maneno
Waliofanikiwa – kirejeshi, makadirio – unominishaji
(2 x ½ = alama 1)
k) Kutambua na kuainisha nomino katika sentensi
mashabiki – kawaida, vigelegele – dhahania, Kocha Manoa – pekee/halisi/maalum, kikosi cha wachezaji – jamii/ kundi/ makundi
(kutambua 3 x ½ = alama 1½, kuainisha 3 x ½ = alama 1½, jumla alama 3)
l) Dhima za vishazi tegemezi
(i) kivumishi – Gari lililonunuliwa limewasili.
(ii) kielezi – Walilima wakishirikiana
(mfano sahihi katika sentensi 2 x 1 = alama 2)
m) Kutunga sentensi mbili kutumia kitawe ‘bunda’
(i) Furushi la vitu kama karatasi, noti: Mwalimu amebeba bunda la karatasi za watahiniwa.
(ii) Anguka/kosa kitu: Wanafunzi waliobunda ktika mtihani walikuwa wazembe.
(Sentensi sahihi 2 x 1 = alama 2)
n) Sentensi moja yenye miundo miwili ya virai husishi
Mtoto wa shule ameketi karibu bustanini.
H+N H+E
(2 x 1 = alama 2)
o) Kuakifisha
Siku ya Kiswahili Duniani iliadhimishwa na wengi. Ilifana.
Au
Siku ya Kiswahili iliadhimishwa na wengi; ilifana.
(herufi kubwa alama 1, viakifishi alama 1; jumla alama 2)
p) Kinza ni kwa pinga na tambua ni kwa jua (elewa/fahamu) ilhali nata ni kwa gandama (shika/jamidi/ganda).
Tanbihi: Ni visawe vinavyolengwa.
(2 x ½ = alama 1)
r) Kutunga sentensi kuonyesha maana ya nahau ‘shika shokoa’.
Maana: Lazimisha mtu kufanya jambo
Mfano: Mwalimu aliwashika shokoa wanafunzi wazembe wakajibu maswali.
(sentensi sahihi 1 x 1 = alama 1/0)
s) Methali inayoafiki muktadha
Mtegemea nundu haachi kunona. (1 x 1 alama 1/0)
t) Kuainisha sentensi kulingana na maana zilizomo
Mkiondoka wawiliwawili, mtafika haraka.
(i) masharti (ii) sisitizi/kariri (iii) arifu/ taarifa
(2 x ½ = alama 1)
4. SWALI LA NNE: ISIMUJAMII
a) Sifa za sajili ya Viwandani
(i) msamiati teule – kutaja bidhaa zinazozalishwa kama sukari
(ii) kuchanganya ndimi – Kiingereza na lugha za kieneo, duty, boiler
(iv) sentensi ndefu katika kutoa taratibu na masharti kazini
(v) maswali yanayohitaji majibu moja kwa moja ili kutaka kujua ukweli kuhusu suala fulani
(vi) maswali ya balagha – Ukichelewa kazini, unataka nini?
(vii) lugha ya maagizo/ uamrishaji – Mtu yeyote asipige simu wakati wa kazi!
(viii) ukali – Hakuna kubembelezana tena!
(ix) kurejelea sehemu za sheria, katiba au mkataba wa kuajiriwa
(x) kauli kamilifu kwa sababu ni lazima kueleweka bila utata
(xi) utohozi – meneja, mashine, trakta
(xii) misimu – Sitaki mtu aniletee!
(xiii) kutozingatia sarufi/lugha legevu – Baadhi ya wafanyakazi huenda hawana kisomo kingi.
(hoja 5 na mifano ambatani x 1 = 5)
b) Sifa za sajili ya mazungumzo ya nyumbani baina ya wanandoa katika dondoo
(i) unyenyekevu kuashiria mapenzi – Polepole Mama Mercy!
(ii) Lugha yenye ahadi – …tutakuwa na muda wa kila kitu
(iii) kutotaja jina halisi mwenza na badala yake kutumiamajina ya watoto – Mama Mercy
(iv) maswali elekezi- Unanilewa…?
(v) kukata kauli – Mama Mercy anamkatiza mwenzake kwa kusema ana njaa.
(vi) kulumbana – Wahusika wote wawili wanazungumza.
(vii) kubadili mada ghafla – Mama Mery amwita Dadii na kusema ana njaa.
(viii) kuchanganya ndimi – bad coincidence
(ix) kauli fupi ambazo sio sentensi – maneno ya Mama Mercy
(hoja 5 na mifano ambatani x 1 = 5)
ADHABU
Ondoa nusu alama kwa kila kosa linalotokea huku ukiweka upeo wa jumla ya makosa ya kuadhibiwa katika kila moja ya maswali hayo manne yaani, Ufahamu, Ufupisho, Matumizi ya Lugha na Isimujamii.
Adhabu kwa makosa ya sarufi na hijai katika kila swali itekelezwe kwa lengo la kumhadharisha mtahiniwa kwamba ni sharti azingatie kanuni za kuandika na sarufi bora ili kuyawezesha mawasiliano kamilifu kwa njia ya maandishi. Hata hivyo, adhabu isiwe na lengo la kumtia hofu mtahiniwa hadi aogope kuandika majibu kwa mtihani. Aidha, adhabu hii itekelezwe mwishoni mwa swali wala sio papo hapo linapotokea kosa. Muhimu zaidi ni kwamba kosa katika kuandika jibu lisiathiri usahihi wa jibu lenyewe.
Huu ndio ukurasa wa mwisho uliochapishwa.